Dalili/Ishara zipi za kutaka kujiua

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Dalili/Ishara_zipi_za_kutaka_kujiua

Kumbuka ya kwamba watu wengine wanaojiua huwa hawaonyeshi dalili zozote za kutaka kujiua kabla ya kujiua. Tena, wengi wao ambao hufa kwa kujiua huonyesha dalili zingine. Kwa hivyo ikiwa wamjua yeyote ambaye anaonyesha dalili zifuatazo za kujiua, fahamu ya kwamba anahitaji usaidizi wa dharura.

  • Mnyogovu au aliye na hasira kila wakati.
  • Anayeongea au kuandika kuhusu kifo au kujiua.
  • Anayejitenga na familia na marafiki.
  • Anayehisi hofu, kupoteza matumaini, hasira, uchungu rohoni na hamaki wakati mwingi.
  • Kubadilika kwa hisia ghafla.
  • Mihadarati na kunywa vileo/pombe kupita kiasi.
  • Kupoteza hamu kwa mambo mengi ya kawaida, hata yale mtu hupenda kuyafanya.
  • Kubadilika kwa tabia ya kulala na kula(kuishiwa na usingizi au kulala zaidi, kupoteza hamu ya kula au kula zaidi).
  • Kuzorota kusikoeleweka kwa utendaji wa kazi kazini na shuleni.
  • Kupeana ovyo mali au vitu vya dhamana na kuandika wosia.

MUHIMU; Kuwa makini na ishara za kujiua. Ni ombi la usaidizi ambalo, kwa bahati mbaya halisikizwi. Wakati mtu anapokuambia ya kwamba anafikiria kujiua, kuwa makini na maneno hayo.

Sources
  • Felicitas Heyne, Psychologist
  • Audiopedia ID: sw020908