Je Lazima nifikirie kuhusu mpango wa uzazi

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Je_Lazima_nifikirie_kuhusu_mpango_wa_uzazi

Wasichana wengi walio na ulemavu hukua bila taarifa kuhusu ngono au mpango wa uzazi. Hata hivyo wanawake wengi walio na ulemavu wanaweza kupata mimba-hata wale wasio na hisia katika sehemu zao za chini za mwili. Kwa hivyo kama unapanga kujamiiana na hutaki kupata mimba, ni lazima utumie njia za kupanga uzazi. 

Hapa kuna baadhi ya miongozo ya kuamua ni njia ipi nzuri kwako:

Iwapo ulikuwa na kiharusi, huwezi kutembea na ni lazima uketi chini au ulale kila mara usitumie njia za homoni, kama vile vidonge, sindano, ama chembechemba za kupandwa mwilini. Huenda zikasababisha matatizo katika chembechembe za mgando wa damu.

Iwapo hauna hisia katika sehemu ya chini ya tumbo, ama una hisia ndogo tu, usitumie anintra-uterine device (IUD) (Kifaa maalumu mfano wa "T" cha kuzuia mwanamke kushika mimba). Kisipo wekwa vyema, au ikiwa kuna uwezekano unaweza kuambukizwa maradhi ya zinaa. Bila hisia hutaweza kutambua kwamba unaugua.

Kama huwezi kutumia mikono yako vyema, huenda ikawa vigumu kwako kutumia vizuizi kama diaphragm, kondomu za kike, au povu. Ikiwa hujisikii vizuri muulize mpenzi wako, huenda akawa na uwezo wa kukuwekea.

Kama ulemavu wako hubadilika kwa muda, huenda ukahitaji kubadilisha mbinu yako ya mpango wa uzazi.

Kondomu au mpira haizuii mimba pekee ila, hukukinga pia kutokana na kuambukizwa na maradhi ya zinaa au virusi vya ukimwi (VVU).

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw011111