Je kuna itikadi zipi kuhusiana na saratani

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Je_kuna_itikadi_zipi_kuhusiana_na_saratani

Kwa kawadia, wanawake hawaendi kumuona mhudumu wa afya au daktari hadi pale ambapo anaumwa sana. Kwa hivyo, wanawake ambao huugua saratani hugonjeka zaidi au hufa kwa sababu saratani hii haipatikani kwa wakati. Pia, wanawake ambao hupatikana na saratani hutengwa na jamii na familia zao na kusemekana kuwa 'wamelaaniwa'. Kutengwa huku sio tu kubaya kwa wanawake wanaougua, bali kwa jamii nzima kwa jumla, kwa sababu huwafanya watu wasijue jinsi saratani huwaathiri watu.

MUHIMU: Saratani sio maambukizi. Sio 'kushika' na haisambazwi kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw011403