Je kuna umuhimu gani kwangu kuiangalia afya yangu katika miaka ya uzeeni

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Je_kuna_umuhimu_gani_kwangu_kuiangalia_afya_yangu_katika_miaka_ya_uzeeni

Jinsi mwili wa msichana mdogo unavyobadilika anapobaleghe, ndivyo mwili wa mwanamke unavyobadilika miaka yake ya kuzaa inapoisha. Kukomaa kwa hedhi na uzee huleta mabadiliko katika nguvu ya mifupa na misuli, na nguvu kwenye viungo na afya kwa jumla.

Mwanamke anaweza kuimarisha hali ya maisha na afya yake katika siku za uzeeni kwa:

  • kula vizuri
  • kunywa maji kwa wingi
  • kufanya mazoezi kila mara
  • kupata matibabu kwa wakati
  • kuhakikisha kuwa hukai bila kufanya lolote
Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010904