Je kwa nini niwe maakini na usalama wangu kibinafsi

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Je_kwa_nini_niwe_maakini_na_usalama_wangu_kibinafsi

Kwa maana mwanamke aliye na ulemavu anaweza kushindwa kujilinda, yuko na uwezekano mkubwa wa kuwa hatarini kuliko mwanamke asiye na ulemavu. Lakini kuna mambo mwanamke anaweza kufanya kujilinda. Yafaa kufanya baadhi ya mazoezi haya katika vikundi vya wanawake walemavu.

Ukiwa katika sehemu ya umma na mtu ajaribu kukuumiza au kukunyanyasa piga kamsa/kelele kadri ya uwezo wako.

Fanya jambo lisilompendeza, kama kutema ute (mate) mwingi, ama kutapika au kufanya jambo la kiwazimu.

Tumia fimbo yako, mkongojo, au kiti cha magurudumu kumuumiza.

Ikiwa ni mtu wa familia yenu, jaribu kumueleza mtu mwingine wa familia unaye muamini. Inaweza pia kufaa kuzungumzia katika vikundi vya kibinafsi vya wanawake walio na ulemavu.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw011112