Je napaswa kujua nini kuhusu siku zangu za hedhi

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Je_napaswa_kujua_nini_kuhusu_siku_zangu_za_hedhi

Angalau mara moja kila mwezi wakati wa ujana wake, mwanamke huwa na siku ambapo hutokwa damu ya hedhi kutoka kwenye tumbo lake, kupitia kwa sehemu yake ya uzazi. Hii huitwa 'hedhi', 'damu ya mwezi' au 'siku za mwezi'. Tukio hili ni jambo la kawaida, na njia moja ya mwili kujitayarisha kwa kushika mimba.

Wanawake wengi huchukulia hedhi kama jambo la kawaida maishani mwao. Lakini, hawaelewi ni kwa nini hufanyika, au ni kwa nini wakati mwingine mabadiliko hutokea.

Siku za mwezi huwa tofauti kwa kila mwanamke. Huanza siku ya kwanza ambapo mwanamke huona damu hii. . Baadhi ya wanawake hupata hedhi baada ya kila siku 28. Kuna wale ambao hupata hedhi baada ya kila siku 20 na wengine kila baada ya siku 45. Kila mwanamke atagundua kuwa, muda unaopita baada ya kila hedhi hubadilika anapozeeka, baada ya kujifungua, au kwa sababu ya mawazo tele.

Viwango vya homoni aina ya 'estrogen' na 'progesterone' ambazo hutengenezwa mwilini mwake hubadilika kila siku ya mwezi. Katika siku za kwanza za mwezi, mwili wake hutengeneza 'estrogen' kwa wingi, ambayo husababisha kunawiri kwa tumbo la uzazi. Mwili hutengeneza nyumba ya mtoto ili mtoto apate mahali laini pa kukua, ikiwa mwanamke atashika mimba mwezi huo.

Siku 14 kabla ya mwisho wa mwezi, wakati tumbo liko tayari, yai hutoka kwenye ovari. Hii huitwa 'ovulation'. Yai hili husafiri hadi likafika kwenye tumbo la uzazi. Wakati huu, mwanamke yuko tayari kushika mimba. Ikiwa mwanamke huyu alishiriki ngono hivi karibuni, basi mbegu ya mwanamume itaungana na yai lake. Hii huitwa 'fertilisation' na ndio mwanzo wa uja uzito.

Katika siku 14 za mwisho wa mwezi-hadi hedhi itakayofuata-mwili wa mwanamke hutengeneza homoni aina 'progesterone'. Homoni hii hutayarisha tumbo kwa uja uzito. Kwa vile katika miezi mingi yai halihaliungani na mbegu, nyumba ya mtoto ilioko ndani ya tumbo lile haihitajiki. Hivyo basi, ovari huacha kutengeneza homoni za 'estrogen' na 'progesterone', na nyumba ya mtoto huanza kunyauka. Wakati ambapo uyoga huo hutoka wakati wa hedhi, yai lile pia hutoka. Ndio mwanzo wa mwezi mpya. Baada ya hedhi, ovari huanza tena kutengeneza 'estrogen' na nyumba ya mtoto hukua.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010215