Je nastahili kufanya nini ili niweze kustahimili dalili za hedhi au Pre-menstrual Syndrome

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Je_nastahili_kufanya_nini_ili_niweze_kustahimili_dalili_za_hedhi_au_Pre-menstrual_Syndrome

Kuna mambo tofauti ya kuzingatia kwa kila mwanamke. Ili kutambua nini haswa kitasaidia, ni wajibu wa kila mwanamke kujaribu kila mbinu. Kwanza kabisa, jaribu mbinu ulizopewa hapo chini kama zitakusaidia wakati wa hedhi.

Mbinu hizi huenda zitakusaidia:

  • Punguza kiwango cha chumvi. Chumvi huufanya mwili kuweka maji mwilini, jambo ambalo hukufanya uhisi kama tumbo limejaa.
  • Epukana na matumizi ya 'caffeine' (hupatikana sana kwenye kahawa, chai na vinywaji kama soda)
  • Jaribu kula njugu, samaki, nyama na maziwa, ama vyakula vingine vyenye wingi wa madini ya protini. Mwili wako unapotumia vyakula hivi, huondoa maji ya ziada yaliyoko mwilini, ili usihisi kama tumbo limejaa.
  • Ni vyema pia kufanya mazoezi.
  • Jaribu pia tiba za mitishamba. Uliza akina mama katika jamii yako ni miti ipi inafanya kazi.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010220