Je naweza kufanya nini ili kupunguza uchungu ambao huja na hedhi

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Je_naweza_kufanya_nini_ili_kupunguza_uchungu_ambao_huja_na_hedhi

Wakati wa hedhi, tumbo hujifinya ili kutoa nyumba ya mtoto. Kujfinya kwa tumbo kunaweza kusababisha maumivu tumboni na mgongoni, wakati mwingine huitwa 'cramps'. Maumivu haya huanza kabla ya hedhi au baada ya hedhi kuanza.

Utafanya hivi:

  • Suguwa tumbo lako. Hii husaidia misuli iliyokunjana kutulia.
  • Weka maji ya moto kwenye chupa au chombo kingine kile na uwekelee kwenye upande wa chini wa tumbo lako au upande wa chini wa mgongo. Pia unaweza kutumia kitambaa ambacho umelowesha ndani ya maji ya moto.
  • Finya nafasi laini iliyoko kati ya kidole cha gumba na cha pili ili kutuliza maumivu mwilini.
  • Kunywa chai iliyotengenezwa na matunda aina 'raspberry', tangawizi au 'chamomile'. Akina mama katika jamii yako wanaweza kukueleza ni aina zipi za chai hutuliza maumivu.
  • Endelea na shughuli zako za kila siku.
  • Jaribu kufanya mazoezi na kutembea.
  • Meza dawa ya kupunguza maumivu. Brufen hufanya kazi vyema haswa kwa maumivu yanayosababishwa na hedhi.
  • Ikiwa hedhi yako ni nzito na hakuna lolote linalofanya kazi, unaweza kutumia tembe za kupanga uzazi kwa muda wa kati ya miezi 6 hadi 12.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010218