Je naweza kufanya nini ili nihisi vyema hedhi inapokomaa

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Je_naweza_kufanya_nini_ili_nihisi_vyema_hedhi_inapokomaa

Hedhi kukomaa ni kawaida. Ingawa akina mama huwa na hisia tofauti wakati huo, wengi hubadilisha lishe na maisha yao kwa jumla.

Hapo zamani, madaktari walipendekeza kuwa akina mama watumie dawa zilizo na homoni za 'oestrogen' na 'progesterone' ili kutuliza makali ya ishara za kukomaa kwa hedhi. Hii inajulikana kama "Hormone Replacement Therapy" yaani HRT. Kwa bahati mbaya, utumizi wa HRT umesababisha hatari ya saratani ya matiti, ugonjwa wa moyo, damu kuganda na kiharusi. Akina mama wametahadharishwa kutotumia dawa hizi.

Ikiwa unapata ishara zinazokupatia wasiwasi, jaribu kufanya yafuatayo:

Vaa nguo ambazo unaweza kuvua kwa urahisi ukianza kutokwa na jasho.

Usitumie pombe, wala kula vyakula vilivyotiwa pilipili. Hivi vinaweza kusababisha uhisi joto.

Usinywe kahawa au chai nyingi. Vinywaji hivi vina 'caffeine' ambayo hukufanya uhisi wasiwasi na hata hufanya ukose usingizi.

Fanya mazoezi kila mara.

Kama wewe hutumia pombe, kunywa kiasi kidogo tu. Pombe huongeza kiwango cha hedhi na vipindi vya joto mwilini.

Acha kuvuta sigara na kutafuna tumbaku. Vitu hivi vinaweza kusababisha kubadilika kwa hedhi yako na pia kuidhoofisha mifupa yako.

Hakikisha kuwa unaielezea familia yako kuwa hisia zako zitabadilika kwa urahisi. Pia itasaidia kuzungumzia hisia zako na akina mama wengine ambao wako katika hali ya hedhi kukomaa.

Uliza kuhusu utumizi wa dawa za kienyeji katika jamii yako. Kwa kawaida, akina mama ambao tayari wamepitia kukomaa kwa hedhi, watajua jinsi ya kukusaidia.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010903