Je nawezaje kufanya mazoezi ya kufinya

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Je_nawezaje_kufanya_mazoezi_ya_kufinya

Zoezi hili laweza kusaidia kuimarisha misuli dhaifu ambayo hupitisha mkojo mara nyingi au kuvuja mkojo. Kwanza fanya mazoezi ukiwa unakojoa. Wakati mkojo unapotoka nje, shikioia mkojo kwa kukaza misuli katika uke wako.

Hesabu moja hadi kumi, kisha pumzisha misuli ndiyo mkojo itoke nje. Jaribu kurudia mara kadhaa wakati wowote wa haja ndogo. Baada ya kujua jinsi ya kufanya hili zoezi, finya mara kadhaa wakati wa mchana. Hakuna mtu atajua. Jaribu kufanya haya mazoezi angalau mara nne kwa siku, finya misuli yako mara tano hadi kumi kila wakati.

Baadhi ya wanawake wanaweza kuhitaji upasuaji ili kusaidia kudhibiti kutokwa na mkojo. Kama mkojo wako unavuja sana na zoezi hili halisaidii, pata ushauri kutoka kwa Mtaalamu wa afya katika pahali pa afya ya wanawake. Zoezi hili la kufinya ni nzuri kwa wanawake wote kufanya kila siku. Kwani husaidia kuweka misuli imara na yaweza kuzuia matatizo baadaye katika maisha.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010706