Je nawezaje kuzuia shida za kiafya zinazotokana na moshi

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Je_nawezaje_kuzuia_shida_za_kiafya_zinazotokana_na_moshi

Ili kupunguza hewa yenye moshi unayopumua:

Pikia mahali ambapo kuna hewa ya kutosha. Ikiwa huwezi kupikia nje, hakikisha kuwa kuna amadirisha mawili kwenye chumba hicho. Hii huleta hewa safi, ili moshi uondoke.

Mnaweza kupika kwa zamu na wanawake wengine. Hivi, kila mwanamke atapumua moshi kidogo.

Tafuta njia mbadala za kutayarisha chakula ambazo hucukua muda mfupi (lakini chakula kinaiva). Hivi, utapumua moshi kidogo, na utatumia kuni chache.

Chakula hupikika haraka ikiwa:

  • utakata chakula chenyewe kwa vipande vidogo.
  • utafunika sufuria unachopikia.
  • loweka vyakula kama maharagwe usiku kucha, kabla ya kupika.
  • linda moto wako kutokana na upepo. Tengeneza namna ya kiota kuuzuka moto wako kwa kutumia mawe, udongo au mabati ili sufuria upate moto.
  • linda kuni zisinyeshewe

Tumia jiko ambazo hutoa moshi kidogo. Hii ni njia nzuri ya kuzuia shida za kiafya ambazo husababishwa na moshi unapopika. Jiko ambazo hutumia kuni chache hutoa moshi kidogo na zinapatikana katika maeneo unamoishi, lakini zinaweza kutengenezwa na vifaa vya kiasili.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw030105