Je ni lishe aina gani itasaidia kunipa afya njema katika siku za uzee

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Je_ni_lishe_aina_gani_itasaidia_kunipa_afya_njema_katika_siku_za_uzee

Mwanamke bado anahitaji chakula kilicho na afya anapozeeka, ili kuupa mwili wake nguvu za kuweza kupambana na magonjwa. Kwa vile mwili wake sasa unatengeneza 'estrogen' kidogo, ni vyema kula vyakula vilivyo na wingi wa homoni hii kama vile maboga aina ya maharagwe, soya, ndengu na aina zingine za maharagwe. KWa vile mifupa yake inapoteza uzito wake anapoendelea kuzeeka, ni vyema ale vyakula vilivyo na wingi wa madini aina 'calcium" ambao husaidia kuimarisha mifupa.

Wakati mwingine, watu wazee huwa hawana hamu ya kula kama hapo awali. HIi husababishwa na ladha na harufu, ambayo hufanya kula kuwa shida sana. Wakati mwingine mabadiliko yanayoletwa kutokana na kuzeeka humfanya mtu ajihisi kuwa ameshiba baada ya kuanza tu kula. Lakini hii haimaanishi kuwa watu wenye umri mkubwa hawahitaji chakula kilicho na afya. Wanahitaji kuhimizwa kuendelea kula vyema, na kula vyakula aina tofauti tofauti.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010905