Je ni vipi ambavyo naweza kusafisha maji ya kunywa

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Je_ni_vipi_ambavyo_naweza_kusafisha_maji_ya_kunywa

Hapa kuna maelezo ya jinsi ya kusafisha maji:

Jua Miale ya jua huua viini hatari. Ili kusafisha maji kwa kutumia jua, jaza maji kwenye glasi safi au chupa ya plastiki, na uiache nje kwenye jua mchana kutwa. Hakikisha kuwa umeweka vyombo hivi mahali palipo wazi kama vile paa ya nyumba. (Ikiwa maji ya kunywa yatahitajika mara moja, weka vyombo hivi kwenye jua kwa muda wa masaa 2 - haya yanatosha kwa kusafisha maji).

Ili kuzuia maji kuingiwa viini, tafuta mahali palipo mabli na watoto, vumbi na wanyama. Ikiwa unataka maji yapoe kabla ya kunywa, weka vyombo vyenye maji haya ndani ya nyumba usiku kucha. Maji yanaweza kuhifadhiwa kwa siku moja au mbili yakiwa ndani ya vyombo hivi. Kusafisha maji kwa kutumia miale ya jua husaidia sana katika maeneo ya jua kali.

Maji ya Ndimu Wakati mwingine, maji ya ndimu huua viini vya kipindupindu (na viini vingine). Ongeza vijiko 2 vya maji ya ndimu kwalita moja ya maji na uyaache yatulie kwa dakika 30.

Kuchemsha Kuchemsha maji kwa dakika 5 huua viini. Wacha maji yachemke kwa dakika 5 kabla ya kuepua sufuria. Kwa vile kuchemsha maji hutumia raslimali nyingi, tumia njia hii ikiwa tu hauna njia nyingine ya kusafisha maji.



Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010118