Je ni vipi ambavyo usafi unaweza kuzuia kusambaa kwa viini vya magonjwa

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Je_ni_vipi_ambavyo_usafi_unaweza_kuzuia_kusambaa_kwa_viini_vya_magonjwa

Usafi katika jamii (haswa ikizingatiwa kuwa na vyoo safi), usafi pale nyumbani, usafi wa mtu binafsi, yote ni muhimu ili kuzuia magonjwa kwa kuzuia kusambaa kwa viini vya magonjwa.

Kwa mfano:

  • Mtu aliyeambukizwa viini akihara hadharani.
  • Nguruwe kula kinyesi cha mtu huyo.
  • Mojawapo ya watoto wa mtu yule akianza kucheza na nguruwe yule, na kujipaka kinyesi kile.

Baadaye, mtoto yule hulia, kisha mamake ambembeleze na kusafisha vidole vyake kwa kuvipangusa akitumia nguo yake. Kinyesi kile kinajipaka kwenye mikono ya mama.

Kwa vile mama yule ana shughuli nyingi ya kuitayarishia familia yake chakula, anasahau kuosha mikono yake kabla ya kuanza kupika. Anatumia nguo yake kushikilia sufuria ili asichomoke mikono, huku akisahau kuwa nguo hiyo sio safi.

  • Familia yake hula chakula kile. Kisha kila mtu wa familia hiyo huhara.
  • Kama familia ile ingetumia tahadhari zilizopo hapa, kusambaa kwa ugonjwa huu ungezuiwa.
  • Ikiwa baba huyo angetumia choo
  • Ikiwa nguruwe hangeruhusiwa kuzurura
  • Ikiwa mama huyo hangetumia vazi lake kuipanguza mikono ya mwanawe kisha aguze chakula.
  • Ikiwa mama huyo angenawa mikono baada ya kumshika mwanawe na kabla ya kupika chakula.
Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010105