Je nijiepushe na madawa yapi ili kuhakikisha kuwa afya yangu ni njema

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Je_nijiepushe_na_madawa_yapi_ili_kuhakikisha_kuwa_afya_yangu_ni_njema

Kuna madawa aina tofauti ambayo hutumika kila siku. Katika sehemu zingine, madawa au pombe ambazo hupikwa huwa na ishara takatifu katika tamaduni nyingi. Katika maeneo fulani, vileo kama vile mvinyo au pombe kwa kawaida huandaliwa pamoja na chakula. Madawa na pombe hutumika sana nyakati za sherehe. Pia, kuna madawa ambayo hutumika kama dawa. Watu wengi hawafahamu kuwa pombe na tumbaku ni madawa hatari.

Baadhi ya madawa ambayo hutumika kwa njia isiyofaa ni:

  • pombe: vileo kama vile pombe, mvinyo, na pombe kali
  • cocaine, heroin, opium, methamphitamine
  • tambuu, miraa, matawi ya tumbaku
  • bangi na hashish
  • tembe ambazo humwezesha mtu kupunguza uzito au kumsaidia kukaa macho
  • tembe, hasa zile za kutuliza maumivu makali, au zinazomsaidia mtu kupata usingizi au kupumzika
  • gundi, mafua aina petroli


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010302