Je ninawezaje kujilinda wakati wa hedhi

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Je_ninawezaje_kujilinda_wakati_wa_hedhi

Akina mama wengi hutengeneza sodo kwa kutumia viraka au pamba ili kushikilia ile damu ya hedhi. Viraka hivi hushikiliwa kwa mshipi, kipini au suruali ya ndani. Ni muhimu sodo hizi kubadilishwa mara kadhaa kwa siku, na kuoshwa vizuri kwa kutumia sabuni na maji ikiwa vitatumika tena.

Akina mama wengine hutumia kifaa fulani ambacho wao huingiza kwenye sehemu yao ya uzazi ambacho wao hununua au kutengeneza kwa kutumia pamba, kitambaa au sifongo (sponge). Vifaa hivi huitwa 'tampons'. Ikiwa unatumia 'tampons' hakikisha kuwa unabadilisha angalau mara mbili kwa siku. Usipofanya hivi, huenda ukapaata maambukizi hatari.

Osha sehemu zako za uzazi kwa kutumia maji kila kila siku ili kuondoa damu iliyosalia. Tumia sabuni. Ni jambo muhimu kuoga wakati wa siku zako za hedhi.

Unaweza kuendelea na kazi zako za kila siku. Kufanya mazoezi kunaweza kupunguza uchungu ambao wanawake wengine huhisi wakati huu.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010114