Je nini cha muhimu kufahamu kuhusu msongamano wa mawazo au kukosa raha au kutokuwa na hisia zozote

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Je_nini_cha_muhimu_kufahamu_kuhusu_msongamano_wa_mawazo_au_kukosa_raha_au_kutokuwa_na_hisia_zozote

Watu wengine hutambua huzuni kama "kuwa na uzito moyoni" au "kupoteza roho au nafsi".

Ni kawaida kwa mtu kuwa na hisia za huzuni anapompoteza ampendaye. Lakini, ikiwa amekuwa na ishara zifuatazo kwa muda mrefu, basi ana shida za kiakili:

Ishara:

  • kuwa na hisia za huzuni wakati wote
  • shida kupata usingizi au kulala sana
  • anapata shida kufikiria sawasawa
  • hana hamu tena ya shughuli kama kula au ngono
  • shida za kiafya kama vile kuumwa na kichwa, shida za tumbo, ambazo hazisababishwi na ugonjwa
  • kufanya mambo na kuzungumza polepole
  • hana nguvu ya kufanya chochote
  • fikira za kifo au kujitoa uhai

Huzuni inaweza kumfanya mtu akajitoa uhai. Takribani kila mtu huwa na fikira za kujitoa uhai wakati mmoja. Lakini fikira hizi zikija kwa wingi mara kwa mara, lazima mwanamke huyo apate usaidizi haraka.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw011508