Je nitajuaje ikiwa niko na maziwa ya kutosha na kama maziwa yangu ni mazuri

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Je_nitajuaje_ikiwa_niko_na_maziwa_ya_kutosha_na_kama_maziwa_yangu_ni_mazuri

Wanawake wengi hudhania kwamba hawana maziwa ya kutosha. Hakika, si kweli. Hata akina mama wasiokula chakula cha kutosha kwa jumla huwa na maziwa ya kutosha kwa watoto wao.

Kiwango cha maziwa ambacho matiti hutengeneza (hifadhi yako ya maziwa) hutegemea kiasi ambacho mtoto hunyonya. Jinsi anavyozidi kunyonya, ndivyo maziwa yanavyozidi kutengenezwa. Ukikosa kumpa matiti na badala yake ummpe maziwa kwa chupa, mwili wako utatengeneza maziwa kidogo.

Wakati mwingine yaweza kuonekana kana kwamba mtoto anataka kunyonya kila mara. Ukimpa mtoto maziwa kila anapohisi njaa, maziwa yako yataongezeka. Siku chache zitakazofuata mtoto ataonekana ni kana kwamba ameshiba. Kunyonyesha mtoto usiku kunasaidia kuongeza kiwango cha maziwa ya mama. Jizuie kumuamini yeyote yule - hata mhudumu wa afya - anayekuambia hauna maziwa ya kutosha.

Matiti hayahitaji kuwa makubwa ili kutengeneza maziwa. Mama anavyozidi kunyonyesha watoto zaidi, atahisi matiti yamepungua saizi. Matiti madogo yaweza kutengeneza kiwango sawa cha maziwa yanayotengezwa na matiti makubwa.

Mtoto anapata maziwa ya kutosha iwapo:

  • anakua vyema, na anaonekana mwenye furaha na afya.
  • hukojoa mara 6 au zaidi na huenda choo kubwa karibu mara 1 hadi 3 mchana na usiku. Mara nyingi unaweza kubaini hili mtoto akishafikisha siku 5, atakapoanza kukojoa na kwenda choo kubwa mara kwa mara. Mtoto aliyefikisha wiki 2 huenda asiende choo kubwa kila siku. Iwapo mtoto anakula vyema, anakojoa na anaonekana kuridhika, choo kitakuja.

Kwa sababu sura ya maziwa ya mama huonekana tofauti na maziwa mengine, wanawake wengine huhofia sio maziwa mazuri. Lakini maziwa ya mama humpa mtoto lishe yote anayohitaji.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010809