Je nitashughulikia vipi chakula cha mtoto

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Je_nitashughulikia_vipi_chakula_cha_mtoto

Tahadhari sana unapotayarisha chakula cha watoto wadogo. Lazima chakula chao kitayarishwe upya kila mara na kiliwe mara moja, wala kisiachwe kilale.

Maziwa ya mama yanaweza kuhifadhiwa kwa masaa manane katika chombo kisafi kilichofunikwa. Ikiwa watoto wakubwa watapewa maziwa ya ng'ombe, lazima yachemshwe ili kuua viini.

Chakula kibichi au kilichosalia baada ya kupikwa na kuliwa ni hatari sana. Chakula kibichi kinapaswa kuoshwa au kupikwa. Chakula kilichopikwa lazima kiliwe mara moja au kipashwe moto kabla ya kula.

Lazima kuku na bidhaa zake zipikwe kabisa ili kuzuia kuenea kwa mafua ya ndege yaani 'avian flu'.

Lazima mboga na matunda yaoshwe au kutolewa maganda kwa kutumia maji safi, haswa ikiwa yataliwa yakiwa mabichi. Mboga na matunda hutibiwa kwa kutumia kemikali kama vile dawa za kuua wadudu na za kuua magugu, ambazo huwa hatari.

Nawa mikono ukitumia sabuni na maji baada ya kushika chakula kibichi. Chakula kibichi, haswa nyama ya ndege wanaoliwa na nyama ya samaki wa baharini, kwa wakati mwingi huwa na viini. Chakula kilichopikwa kinaweza kupata viini ikiwa kitaguzana na chakula kibichi, na viini hivi hukuwa haraka ndani ya chakula kilichopikwa. Chakula kibichi kinastahili kuwekwa kando au mbali na chakula kilichoiva. Visu, mbao ya kukata chakula na mahali unapotumia kuandaa mapishi iwe safi kwa kuoshwa na sabuni na maji baada ya kuandaa chakula.

Sources