Je nitazuiaje mishipa kufura

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Je_nitazuiaje_mishipa_kufura

Mishipa ya rangi ya samawati inayofura kwenye miguu na katika njia ya uzazi huitwa 'varicose veins'. Hii hutokea kadri mtoto anavyoendelea kukua. Mishipa hii inaweza kuwa mikubwa na yenye uchungu mwingi.

Namna ya kuzuia:

  • Usisimame kwa muda mrefu sana. Ikiwa lazima usimame, tembea au songesha miguu kidogo. Wakati umeketi, hakikisha kuwa unainua miguu yako mara kadhaa.
  • Hakikisha kuwa unatembea kila siku. Ikiwa una ulemavu na huwezi kutembea, zungumza na mojawapo wa jamaa zako wakusaidie kufanya mazoezi ya miguu.
  • Ikiwa shida hii imezidi, funga miguu yako kwa kutumia vitambaa. Anza kwa kufunga vitambaa hivi kwenye kifundo cha mguu hadi chini ya goti. Kaza kitambaa katika kifundo cha mguu lakini ulegeze pale chini ya goti. Toa vitambaa hivi usiku.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010710