Je shida gani hujitokeza kwa kula vyakula visivyofaa au chakula kingi

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Je_shida_gani_hujitokeza_kwa_kula_vyakula_visivyofaa_au_chakula_kingi

Wanawake ambao hawapati lishe bora, hasa ikiwa niwanene mno na chakula chao kina wingi wa mafuta au sukari, ni rahisi sana kwao kuugua kutokana na shinikizo la damu, ugonjwa wa moyo, kiharusi, gallstones, kisukari na baadhi ya saratani. Kuwa mnene sana pia kunaweza kusababisha 'arthritis' kwenye miguu.

Hakikisha kuwa unafanya mazoezi ya kutosha, kula mboga na matunda kwa wingi. Hapa kuna mapendekezo ya kupunguza vyakula visivyofaa:

  • tumia maji kwa kupika badala ya kutumia siagi, mafuta ya ng'ombe au mafuta ya nguruwe.
  • toa mafuta kwenye nyama kabla ya kuipika. Usile ngozi ya kuku au bata mzinga.

Epuka vyakula vilivyohifadhiwa ambavyo vina wingi wa mafuta na chumvi, kama vile vibanzi, crisps na soda kama vile Coca Cola.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010420