Je uchunguzi wa virusi vya HIV hufanyikaje

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Je_uchunguzi_wa_virusi_vya_HIV_hufanyikaje

Virusi vya HIV vinapoingia mwilini, mwili huanza kutengeneza chembechembe za kupambana na virusi hivi mara moja. Chembechembe hizi huonekana mwilini wiki 2 au 4 baadaye.

Uchunguzi wa virusi vya HIV hutafuta chembechembe hizi kwenye damu. Uchunguzi wa virusi vya HIV ndio njia ya pekee ya kujua ikiwa mtu ameambukizwa na virusi vya HIV. SIo uchunguzi wa UKIMWI.

Mtu anaweza kufanyiwa uchunguzi wa haraka katika vituo vya afya na hospitali kwa gharama ndogo kabisa. Utapata matokeo ya uchunguzi siku hiyohiyo.

Ukipatikana na virusi hivi baadaya ya uchunguzi, inamaanisha kuwa umeambukizwa virusi hivyo na mwili wako umetengeneza chembechembe kinyume cha virusi vya HIV. Hata ingawa unajihisi mzima, unaweza kusambaza virusi hivi kwa watu wengine.

Ikiwa uchunguzi unaonyesha hauna virusi, kuna 1 ya mambo 2:

  • haujaambukizwa virusi vya HIV, au
  • umeambukizwa hivi karibuni lakini mwili wako bado haujatengeneza chembechembe za kutosha kinyume na HIV ili kuonyesha kuwa umeambukizwa.

Ikiwa umechunguzwa na kupatikana kuwa hauna virusi vya HIV lakini unafikiri kuwa umeambukizwa, lazima ufanyiwe uchunguzi mwingine baada ya wiki 6. Wakati mwingine inabidi uchunguzi urudiwe ikiwa utaonyesha kuwa umeambukizwa. Mhudumu wa afya anaweza kukupa ushauri.

TAHADHARI: Uchunguzi ukionyesha kuwa hauna virusi vya HIV, huja ukiwa unasema 'negative'. Unaweza kuambukizwa ikiwa hautajikinga. Tumia mipira wakati unashiriki ngono.

Ucunguzi wa virusi vya HIV lazima ufanywe:

  • kwa idhini yako.
  • kwa kupewa ushauri kabla na baada ya uchunguzi.
  • kwa njia ya siri. Hakuna mwingine anayefaa kujua matokeo isipokuwa wewe na wale ungependa wajue.
Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw011009