Je upungufu wa damu ni nini

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Je_upungufu_wa_damu_ni_nini

Mtu aliye na upungufu wa damu, ana damu dhaifu. Hii hufanyika chembechembe nyekundu za damu zinapopotea haraka kuliko mwili unavyotengeneza zingine. KWa sababu wanawake hupoteza damu waakti wa hedhi, upungufu wa damu hupatikana sana katika wanawake ambao wamebaleghe na wale ambao hedhi imekomaa. Takribani nusu ya wanawake waja wazito ulimwenguni kote wanaugua upungufu wa damu mwilini, kwa sababu wanahitaji damu ya ziada kwa mtoto anayekua.

Upungufu wa damu mwili ni ugonjwa hatari. Humfanya mwanamke kupata mambukizi mengine, na pia huathiri uwezo wake wa kufanya kazi na kusoma. Wanawake wanaugua upungufu wa damu mwilini wanaweza kuvuja damu sana au kufa wakati wa kujifungua.

Je, nini ishara za upungufu wa damu mwilini?

  • macho, makucha na ndani ya midomo kukosa rangi
  • udhaifu na kujihisi asiye na nguvu
  • kizunguzungu, hasa unapoamka ikiwa umelala au umeketi
  • kuzimia
  • kupungukiwa hewa
  • moyo kupiga kwa kasi
Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010415