Jinsi gani kufanya kazi na maji yaathiri afya yangu

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Jinsi_gani_kufanya_kazi_na_maji_yaathiri_afya_yangu

Wanawake lazima kila wakati watafute na wabebe maji kwa familia zao. Wanawake pia hufua na kufanya usafi kila wakati, na wao pia ndio huwaosha watoto. Kazi hizi zote ni muhimu kwa afya ya mwanamke na ya familia yake. Ingawaje, kazi zizi hizi zaweza kusababisha shida za kiafya.

Shida za kiafya zinazotokana na kufanya kazi na maji:

Wanawake wanaotumia mda mwingi kwenye maji machafu wako katika uwazi wa vimelea na wadudu wanaoishi ndani na karibu kwenye maji. Wanawake hawa wanaweza pata 'bilharzia', 'guinea mdudu', wadudu wanao sababisha upofu wa mto na kipindupindu na magonjwa mengineyo ya vimelea

Wanawake wanaoishi kwenye mitaro inayotoka kwa kampuni au mashamba makubwa wanaweza kuwa wazi kwa kemikali kwenye maji. Kemikali yanaweza sababisha mashida mengi za kiafya.

Maji ni mojawapo ya vitu vizito ambavyo wanawake lazima wabebe, kwa hivyo kuteka na kubeba maji inaweza sababisha shida ya mgongo na shingo, na pia shida zinginezo za kiafya.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw030111