Kuna umuhimu gani kwa mimi kama mwanamke kujikinga kutokana na virusi vya Ukimwi na Ugonjwa wa Ukimwi

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Kuna_umuhimu_gani_kwa_mimi_kama_mwanamke_kujikinga_kutokana_na_virusi_vya_Ukimwi_na_Ugonjwa_wa_Ukimwi

Virusi vya ukimiwi na ukimwi ni tofauti kwa wanawake kwa sababu:

Wanawake huambukizwa virusi vya ukimwi au HIV kwa urahisi ikilinganishwa na wanaume kwa sababu, wakati wa tendo la ngono mwanamke ndiye 'anapokea'. Hii inamaanisha kuwa shahawa ya mwanaume husalia kwenye sehemu ya uzazi ya mwanamke kwa muda mrefu. Ni ikiwa kuna virusi vya HIV kwenye shahawa, basi kuna uwezekano mkubwa vitangamane na damu yake kupitia sehemu yake ya uzazi, hasa ikiwa kuna vidonda au magonjwa ya zinaa.

Wanawake huambikizwa wakati wangali na umri mdogo kuliko wanaume. Hii ni kwa sababu wasichana wadogo kwa mara nyingi hawana uwezo kukataa kushiriki ngono bila kinga, na mara ngingi huolewa mapema kwa wanaume wenye umri mkubwa, ambao wamekuwa na nafasi nyingi za kuambikizwa.

Mara ngingi akina mama huishi bila kutibiwa magonjwa ya zinaa. Hii hufanya ikawa rahisi kuambukizwa virusi vya ukimwi.

Akina mama kuongezewa damu zaidi ya wanaume kwa sababu ya shida wakati wa kujifungua.

Lishe mbaya na udhaifu kutokana na uzazi huwafanya wanawake kushindwa kupigana na magonjwa.

Akina mama hulaumiwa visivyo kwa kusambaza UKIMWI, hata ingawa wanaume wengi hawataki kutumia kondomunau mipira au kupunguza idadi ya wapenzi wao.

Mwanamke aliyeambukizwa virusi vya ukimwi anaweza kumuambukiza mtoto wake.

Akina mama ndio huwatunza jamaa ambao wanaugua UKIMWI, hata kama wao wenyewe ni wagonjwa.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw011006