Kwa nini pombe na mihadarati ni hatari kwa mwanamke

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Kwa_nini_pombe_na_mihadarati_ni_hatari_kwa_mwanamke

Pamoja na shida ambazo anayetumia mihadarati hupata, wanawake hupata shida maalum:

Wanawake ambao hunywa pombe kupita kiasi au kutumia mihadarati wana uwezekanao mkubwa wa kuugua maradhi ya maini zaidi ya wanaume.

Wanawake na wasichan wengi huhadaiwa kushiriki ngono, wanapotumia pombe au mihadarati. Hii husababisha mimba zisizotakikana, maambukizi ya virusi vya HIV au magonjwa mengine ya zinaa.

Mwanamke mja mzito anakunywa pombe, kuvuta sigara au kutumia mihadarati, mtoto wake vile vile. Ikitumiwa wakati wa uja uzito, mihadarati na pombe inaweza kusababisha mtoto kuzaliwa na ulemavu na shida zaz kiakili kama vile:

  • shida za moyo, mifupa, sehemu za uzazi, kichwa na uso.
  • uzani mdogo wakati anapozaliwa.
  • anakua pole pole.
  • shida za kimasomo na akili punguani.
  • shida za nidhamu.
  • mtoto pia anaweza kuzaliwa akiwa na uraibu wa mihadarati na kuugua kutokana na kutopata mihadarati hiyo kama mtu mzima.

Wanawake huona aibu zaidi: Katika jamii nyingi, tabia ya wanawake huchunguzwa sana hadharani kuliko ile ya wanaume. Mara nyingi, ni sawa kwa mwanaume kutumia mihadarati na pombe, lakini sio kwa wanawake. Ikiwa mwanamke atashindwa kudhibiti tabia yake kwa sababu ya utumizi kupita kiasi wa pombe au mihadarati, yeye huonekana kama mwanamke asiye na heshima, hata ingawa hashiriki ngono na wanaume wengine. Ili kuepuka aibu ambazo huja na kunywa pombe au kutumia mihadarati hadharani, mwanamke anaweza kunywa pombe na kutumia mihadarati kwa siri kwa muda mrefu, badala ya utumizi wa mara moja. Anapokunywa pombe kwa njia hii, anaweza kudhibiti tabia yake, na kuweka siri utumizi mbaya. Tabia hizi zote huongeza hatari inayotokana na utumizi mbaya wa pombe na mihadarati.

Utumizi mbaya wa pombe na mihadarati hufanya hali mbaya kuwa mbaya zaidi, hasa pale nyumbani: Wanawake ambao wapenzi wao hutumia pombe au mihadarati vibaya hupata majeraha na hata hufa.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010307