Kwa nini wanawake walio na ulemavu mara nyingi hukosa kujithamini

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Kwa_nini_wanawake_walio_na_ulemavu_mara_nyingi_hukosa_kujithamini

Wanawake walio na ulemavu mara nyingi hukataliwa. Hukataliwa kama washirika wanaofaa katika ndoa ama huonekana kama picha isiyofaa katika sehemu za kazi.

Wasichana na akina mama walio na ulemavu mara nyingi huwa hawana uwezo wa kupata elimu, japo masomo yanapatikana. Kwa mfano, hata katika skuli maalumu za watoto walio na ulemavu, wavulana hupewa nafasi za kwanza.

Wanawake walio na ulemavu wako na uwezekano wa kukosa kupata mafunzo ya ujuzi ya kazi ya aina yoyote. Wao hudhalilishwa-kimwili, kihisia na kimapenzi. Kinyume na wanaume na wanawake wasio na ulemavu, ni nadra kuruhusiwa kufanya maamuzi nyumbani au katika jamii.

Wanawake walio na ulemavu hufunzwa kutojithamini na jamii. Wao huonekana kama wasioweza kukidhi mwanaume, kuzaa watoto na wasio weza kufanya kazi yoyote ya thamani. Nkwa hivyo hawathaminiwi. Hata familia zao huwatilia maanani tu, wanapo jizatiti na kuonyesha umuhimu wao.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw011104