Kwanini titi ni bora kwa mtoto wangu

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Kwanini_titi_ni_bora_kwa_mtoto_wangu

Kunyonyesha mtoto ni moja ya desturi kongwe na bora zaidi kiafya duniani. Lakini ulimwengu unavyobadilika, wanawake wakati mwingine huhitaji habari na usaidizi ili kuendelea kunyonyesha watoto wao.

Kunyonyesha mtoto ni muhimu kwa sababu:

  • Maziwa ya mama ndicho chakula pekee sahihi cha kumsaidia mtoto kukua katika afya nzuri na imara.
  • Kunyonyesha mtoto husaidia mfuko wa uzazi kuacha kutoa damu baada ya mtoto kuzaliwa.
  • Maziwa ya mama humkinga mtoto dhidi ya maradhi na maambukizi kama vile kisukari, saratani, kuhara, na homa ya mapafu. Kinga ya mama dhidi ya magonjwa hupitishwa hadi kwa mtoto kupitia maziwa yake.
  • Kunyonyesha mtoto husaidia kumkinga mama dhidi ya magonjwa kama saratani na mifupa dhaifu ama iliyo haraka kuvunjika (osteoporosis).
  • Mwanamke anapomnyonyesha mtoto wake, maziwa huwa safi, tayari na yenye joto la sawa wakati wote.
  • Kunyonyesha husaidia mama na mtoto kuhisi kuwa karibu na salama.
  • Kwa baadhi ya wanawake, kuwapa watoto wao maziwa pekee yake kunaweza kuwasaidia kutoshika mimba nyngine haraka.
  • Kunyonyesha mtoto ni bure.
Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010802