Mbona niamini hisia zangu
From Audiopedia - Accessible Learning for All
QR for this page
Wanawake wengi hufundishwa wakiwa wachanga jinsi ya kuwa wakarimu na kujaribu kutomkosea mtu yeyote.
Kwa hivyo, mtu akifanya jambo ambalo humfanya mwanamke kuwa na wakati mgumu/wasiwasi, mara nyingi huwa na wakati mgumu kufanya jambo kutokana na hisia zake.
Lakini kuwa mwangalifu ikiwa:-
Inaweza kuwa vigumu kufanya uamuzi wako kutokana na hisia hizi kwa sababu unaweza kuogopa vile watu wengine watakavyofikiria. Kwa kuongezea hayo, ikiwa unamjua au kumjali mtu huyo unaweza kutokubali kuwa anaweza kukudhuru. Lakini ni vyema uamini hisia zako na uachane na hali yoyote ile ambayo haikuridhishi kabla ya jambo baya kufanyika.
Amini hisia zako. Ni vyema kumkosea mtu ikiwa una makosa kuliko kubakwa.