Mbona watu huanza kutumia pombe au mihadarati

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Mbona_watu_huanza_kutumia_pombe_au_mihadarati

Kwa kawaida, watu huanza kutumia pombe na mihadarati kwa sababu ya msukumo wa kijamii. Wavulana na wanaume hupata msukumo wa kunywa pombe au kutumia mihadarati ili kudhihirisha kuwa wao ni wanaume. Mwanaume huamini kuwa, vile anavyoendelea kunywa, au wingi wa mihadarati anayotumia, ndio inamfanya kuwa mwanaume zaidi. Baadhi ya watu hunywa pombe na kutumia mihadarati kwa sababu ya hisia wanazopata wakiitumia.

Jamii pia imeanza kuwashawishi wasichana na akina mama waanze kunywa pombe na kutumia mihadarati. Huwa wanahisi kuwa wanaonekana kukomaa au watu wa kisasa. Wao hufikiria kuwa watakubaliwa na watu wengine katika jamii.

Kampuni ambazo hutengeneza na kuuza pombe na mihadarati pia hutumia ushawishi wa kijamii. Matangazo ya kibiashara ambayo hufanya matumizi ya mihadarati na unywaji wa pombe kuonekana mtindo wa kisasa, hasa kwa viajana, huwashawishi watu kuinunua. Baadhi ya matangazo, muziki na sinema huwahimiza vijana kunywa na kutumia mihadarati. Wakati kampuni ambazo hutengeneza pombe, au mahali ambapo pombe huuzwa, hufanya ununuzi kuwa jambo rahisi la kufurahisha, watu hutaka sana kununua zaidi. Ushawishi huu ni hatari sana, kwa sababu mara nyingi watu hawaelewi kuwa unawaathiri.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010303