Dalili zipi unapaswa kuziangalia
Jiulize maswali haya:
Je, huwa na wivu unapowaona watu wengine, au hukushtumu kwa madai ya kumdanganya? Ikiwa utajipata unabadili tabia yako kumfanya asione wivu, basi anakukalia.
Je, yeye hujaribu kukuzuia kuwaona maarafiki na familia yako, au kujifanyia mambo mwenyewe? Haijalishi sababu gani anatumia. Anajaribu kukuzuia kupata msaada wao. Itakuwa rahisi kwake kukunyanyasa ikiwa huna mahali pa kwenda.
Je, yeye hukutusi au hukufanyia mzaha mbele ya watu wengine? Unaweza kuanza kuamini kile anasema. Hii inaweza kukufanya uhisi kana kwamba unastahili kutendewa mabaya.
Yeye hufanya nini anapokasirika? Je, huvunja au kutupa vitu? Je, amewahi kukuumiza au kukutishia kukuumiza? Je, amewahi kumpiga mwanamke mwingine?Mambo yote haya yanaonyesha kwamba yuko na shida ya kudhibiti matendo yake.
Je, yeye huhisi kutukanwa na watu walio na mamlaka, kama vile walimu wake, wakubwa, au baba yake? Anaweza kuhisi kuwa hana uwezo. Hii inaweza kusababisha ajaribu kupata uwezo juu ya watu wengine katika maeneo mengine ya maisha yake kwa kutumia vurugu.
Je, yeye hudai kwamba pombe, madawa ya kulevya, au dhiki husababisha anavyofanya? Ikiwa atawekelea lawama kwa kitu kingine, anaweza kusema mambo yatakuwa mazuri atakapopata kazi mpya, kuhama katika mji mpya, au atakapoacha kutumia madawa ya kulevya au pombe.
Je, yeye hukulaumu au kumlaumu mtu mwingine kwa matendo yake, au kukana kwamba yeye hufanya vibaya? Kuna uwezekano wa chini wa kubadilika ikiwa anafikiria kwamba mambo anayoyafanya ni makosa yako.