Faida za upangaji uzazi ni zipi

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Kando na kuokoa maisha, upangaji uzazi uko na faida nyinginezo ambazo ni:

  • Kina mama na watoto huwa na afya bora zaidi, kwa sababu mimba za hatari huepukwa.
  • Kuwa na Watoto wachache inamaanisha kila mtoto anapata chakula cha kutosha.
  • Kungoja kupata watoto inawezesha vijana (wanawake na wanaume) kupata wakati wa kukamilisha masomo yao, kupata kazi na kuchangia zaidi katika familia zao na jamii.
  • Kuwa na watoto wachache hupeana muda zaidi kwenu na kwa watoto wenu.

Upangaji uzazi unaweza kukusaidia wewe na mpenzi wako kufurahia ngono zaidi kwa sababu huogopi mimba zisizopangwa. Pia, mbinu zingine ziko na faida zake za kiafya. Kwa mfano kutumia mpira/ kondomu na spermicides husaidia kukinga uenezaji wa magonjwa ya zinaa, pamoja na virusi vya ukimwi. Mbinu za homoni zinaweza kusaidia utokwaji wa damu usiokuwa wa kawaida na kwa maumivu wakati wa hedhi ambapo mwanamke hutokwa na damu.

Mbinu zote za upangaji uzazi zinazopatikana katika kurasa hii zinatumika na mamilioni ya wanawake. Kwa kweli, mbinu hizi ni salama zaidi kuliko ujauzito na kuzaa.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020404