Imani zipi potovu ambazo zinaweza kuzua migogoro ya familia

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

La kusikitisha ni kwamba, katika nchi nyingi usawa wa kijinsia hautiliwi maanani na kupimana nguvu kati ya waumme na wake bado zipo. Kutotiliwa maanani kwa usawa wa kijinsia chanzo chake ni imani potovu kama ifuatavyo;-

  • Wanaume wako na mamlaka kwa wanawake.
  • Wanawake hawana faida na ni mzigo katika familia zao.
  • Wanaume wako na haki ya mali kushinda wanawake.
  • Kile kinashuhudiwa nyumbani ni suala nyeti.

Familia nyingi huwathamini watoto wa kiume sana kuliko watoto wa kike kwa sababu watoto wa kiume wanaweza kusaidia sana utajiri wa familia, kuwasaidia wazazi wakiwa wazee, kufanya sherehe baada ya wazazi kufariki na kuendeleza jina la familia.

Kutokana na hayo, watoto wa kike hunyonyeshwa kwa muda mfupi na kupewa chakula kidogo na huduma za afya, na kukosa kupata elimu au elimu ya kutosha.

Katika jamii nyingi, mwanamke hawezi kuwa mwenye shamba au kuridhi shamba, kupata pesa au kusifiwa.

Akitalikiwa, anaweza kukatazwa kukaa na watoto wake au vitu vyake. Hata kama mwanamke yuko na haki kisheria, tamaduni za jamii zinaweza kumpa mamlaka kidogo maishani mwake.

Kwa mara nyingi mwanamke hawezi kufanya maamuzi vile pesa za familia zitakavyotumika au lini kupata matibabu ya kiafya na hawezi kusafiri au kuhusika kwa maamuzi ya jamii bila ruhusa ya mumewe.

Wakati wanawake wanaponyimwa mamlaka inabidi wawategemee wanaumme ili kuponea. Fauka ya haya hawawezi kwa urahisi kuitisha vitu ambavyo vitawasaidia kuishi maisha mazuri, huwa wanakosa kufanya maamuzi katika uhusiano na waume wao, kwa wakati mwingi huwa wanashindwa lini au watoto wangapi watakuwa nao, au kujua ikiwa wanaumme wao wako na uhusiano na wanawake wengine.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw021003