Je Beriberi ni nini

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Beriberi ni ugonjwa unaosababishwa na ukosefu wa madini aina 'thiamine' ambayo hupatikana katika vitamini B, ambayo husaidia kugeuza chakula kuwa nguvu inayohitajika mwilini. Kama upungufu wa damu mwilini, beriberi huonekana sana katika wanawake kuanzia wanapobaleghe hadi hedhi inapokomaa, na pia katika watoto wao.

Ikiwa chakula kinacholiwa ni nafaka ambayo maganda yake yametolewa, basi kuna uwezekano wa kuugua beriberi, kwa mfano mchele uliosafishwa au muhogo.

Je, nini ishara ya beriberi?

  • kukosa hamu ya kula
  • udhaifu, hasa kwenye miguu
  • mwili kufura na moyo kuacha kufanya kazi
Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010418