Je Napaswa kufanya nini kuhusiana na magonjwa ya zinaa STIs
Magonjwa ya zinaa husambazwa kwa haraka kutokana na uhusiano wa ngono wa kulazimishwa kwa sababu ngozi ya uke huwa imeraruka. Kama mwanamume aliyekubaka alikuwa na ugonjwa wa zinaa, huenda akakusambazia. Kwa sababu huwezi kujua kama allikuwa ameambukizwa, unastahili kutibiwa ili kuzuia kuambukizwa na kuwaambukiza wengine. Tumia dawa ya Kaswende, Syphilis na Chlamydia na uangalie dalili za magonjwa mengine ya zinaa. Tumia dawa za magonjwa hayo hata kama unafikiri umeambukizwa au la.
Pia Unastahili kufanyiwa uchunguzi wa virusi vya ukimwi. Katika sehemu ambazo virusi vya ukimwi vimesambaa, itakuwa vyema kutumia dawa za kuzuia virusi vya ukimwi kati ya saa 24 hadi 72 baada ya kubakwa. Muone mhudumu wa afya aliye na ujuzi wa maswala ya virusi vya ukimwi, kujua ni dawa zipi zinastahili katika eneo lako. Unastahili kutumia dawa hizo kwa siku 28.