Je UKIMWI husambazwa vipi

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Virusi vya ukimwi hupatikana kwenye majimaji ya mwilini ya watu walioambukizwa - damu, shahawa, maziwa ya mama na maji maji kwenye sehemu ya uzazi ya mwanamke. Virusi hivi husambazwa maji haya yanapoingia kwenye mwili wa mtu mwingine.

Hii inamaanisha kuwa virusu vya ukimwi husambazwa kwa:

  • kushiriki ngono na mtu ambaye ameambukizwa virusi hivi. Hii ndio njia moja ambayo virusi vya ukimwi husambazwa.
  • sindano chafu, au kifaa chochote kile kinachodunga au kukata ngozi.
  • kuongezewa damu, ikiwa damu yenyewe haijafanyiwa uchugnuzi kuhakikisha kuwa haina virusi vya ukimwi.
  • uja uzito, kujifungua au kunyonyesha, ikiwa mama na baba wameambukizwa.
  • kutangamana na damu ambayo imeambukizwa, ikiwa itaingia pahali umekatwa au kidonda cha mtu mwingine.



Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw011004