Je baba wa mtoto wangu anawezaje kunisaidia wakati wa uja uzito na wa kujifungua

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Unapoona kuwa babake mtoto anakujali wakati wa uja uzito hukusaidia sana kimwili na kihisia. Ni muhimu sana ahakikishe kuwa unapata usaidizi kufanya kazi zako. Ikiwa hawezi kufanya baadhi ya kazi hizo mwenyewe, sharti atafute mtu wa kukusaidia. Anaweza pia kuhakikisha kuwa unakula vyakula vya afya, na unaenda kuangaliwa kabla ya kujifungua. Sharti afanyiwe uchunguzi na kutibiwa kwa magonjwa ya zinaa, ikiwemo virusi vya ukimwi Ikiwa anavyo virusi hivyo, ni lazima mtumie mpira wakati wa kushiriki ngono.

Wakati wa kujifungua, baba ya mtoto anaweza pia kuhakikisha kuwa:

  • kuna maji na chakula cha kutosha nyumbani.
  • anamleta mkunga au mhudumu wa afya nyuymbani ili akusaidie wakati wa kujifungua, na kuhakikisha kuwa kuna usafiri wakati wa jambo lolote la dharura.
  • kuwalinda watoto wengine.

Ikiwa atakaa na wewe wakati wa kujifungua, anaweza kukusaidia kwa kukutia moyo. Anaweza kukuambia kuwa mambo yako sawa. Pia anaweza kukupa maji ya kunywa, kukusaidia kutembea au kuchuchumaa wakati wa uchungu wa uzazi au kukusugua mgongo.

Mjulishe baba ya mtoto wako kuwa, wiki 6 za kwanza, baada ya kujifungua ni wakati muhimu sana kwa mwanamke, kujihisi mwenye nguvu na afya. Wakati huu, unahitaji kupumzika na kupata lishe bora. Baba watoto anaweza kukusaidia kupumzika kwa kufanya kazi zingine - kama vile kuteka maji au kutafuta kuni, kuwalinda wale watoto wengine, au kutayarisha chakula. Ikiwa hawezi kusaidia, anaweza kujaribu kutafuta mtu mwingine anayeweza kufanya kazi hizo.

Ni lazima aelewe kuwa ni vyema kutokushiriki kitendo chngono hadi pale ambapo utawacha kutokwa na damu, ili kuzuia kupata maambukizi tumboni.

Hatimaye, ili kuwa na akina mama na watoto wenye afya, ni vyema kusubiri angalau miaka 2 kabla ya kupata mtoto mwingine. Njia moja muhimu ambayo baba ya mtoto wako anaweza kusaidia familia yako kuwa yenye afya ni kwa kutumia dawa za kupanga uzazi. Zungumzia jambo hili na mfanye uamuzi kwa pamoja kuhus mbinu gani mwafaka itakayowafaa. Kisha, shirikianeni kwa kuitumia.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010719