Je dalili za hedhi ni zipi

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Baadhi ya akina mama na wasichana hupata maumivu kabla ya hedhi kuanza. Huenda wanapata ishara mojawapo ya hizi zilizotajwa hapa chini:

  • uchungu kwenye matiti
  • kuhisi kama tumbo limejaa
  • kufura tumbo (inakuwa vigumu kwenda haja kubwa)
  • uchovu
  • uchungu kwenye misuli, hasa upande wa chini wa tumbo na mgongo
  • mabadiliko ya unyevunyevu wa sehemu ya uzazi
  • chunusi usoni
  • hisia ambazo ni vigumu kuzielewa

Wanawake wengi hupata angalau ishara mojawapo ya hizi kila mwezi. Wengine hupata ishara zote. Mwanamke hupata ishara tofauti kila mwezi. Kwa wanawake wengi, siku kadhaa kabla ya hedhi kuanza huwa ni wakati wa wasiwasi mwingi. Hata hivyo, baadhi ya akina mama husema kuwa wao huweza kukamilisha miradi.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010219