Je kiwewe ni nini na kinawezaje kuharibu afya yangu
From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jambo baya linapompata mwanamke au mmoja katika jamii yake, yeye kupatwa na kiwewe. Baadhi ya visa vya kwaida vinavyosababisha kiwewe ni kama vile vurugu nyumbani, ubakaji, vita, kuteswa au majanga.
Kiwewe huhatarisha maisha na afya ya mtu ya kiakili. Humfanya mtu kuhisi hana usalama, mnyonge, na hawezi kumwamini aliye karibu naye wala dunia nzima kwa jumla. Humchukua mwanamke muda mrefu kupata nafuu kutokana na kiwewe, hasa ikiwa kimesababishwa na mtu mwingine na wala sio janga. Mtoto mdogo anapopatwa na kiwewe, kabla hajapata kuelewa nini kilikuwa kinaendelea, au kuzungumzia tukio, linaweza kumuathiri mwanamke bila yeye kujua.