Je kuavyaa mimba ni hatari kwangu

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Kuavyaa mimba kwa njia salama huenda kukakusababishia madhara kuliko kujifungua mtoto.

Kuavyaa mimba ni salama ikiwa kutafanywa:

  • na daktari aliyehitimu na mhudumu mwenye ujuzi.
  • kwa kutumia vifaa vifaavyo.
  • katika mazingira safi. Chochote ambcho huingia ndani ya sehemu ya uzazi au tumbo lazima kiwe kisafi.
  • hadi muda wa miezi 3 (wiki 12) baada ya hedhi ya mwisho.

Kuavyaa mimba sio salama ikiwa kutafanywa:

  • na mtu ambaye hajahitimu.
  • kwa kutumia vifaa au madawa yasiyofaa.
  • katika mazingira chafu.
  • baada ya miezi 3 (wiki 12) za uja uzito, isipokuwa kukifanywa katika kituo cha afya au hospitali ambayo ina vifaa vinavyofaa.

Kila mwaka ulimwenguni kote, takribani mimba milioni 46 hutolewa, hata kama sio halali. Kuavyaa mimba kwa njia isiyo salama kunaweza kusababisha kifo, matatizo kama vila maambukizi, uchungu usioisha, na utasa. Kwa idadi ya wanawake 100, 000 wanaoavyaa mimba kwa njia salama, ni 1 pekee atakwayepoteza maisha. Lakini, kwa idadai ya wanawake 100, 000 wanaoavyaa mimba kwa njia isiyo halali, kati ya wanawake 100 na 1000 watapoteza maisha.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020204