Je kufanya kazi na kemikali kunaweza zorotesha afya yangu

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Wanawake wengi huhusiana na kemikali ambazo zinadhuru bila kujua. Hii ni kwa sababu vitu vingi vya kisasa ambavyo vinatumika nyumbani na kazini huwa na kemikali zisizo tambulishwa kabla matumizi.

Mifano ya vitu ambazo zinadhuru ni kama

  • Dawa za kuangamiza magugu, na wadudu
  • Rangi na kemikali za kutoa, kuyeyusha ama kunyanganya rangi
  • Mafuta na rangi ya vyombo iliyo na chuma risasi
  • Vitu za kuosha vilivyo na dawa ya kupausha ama klorini na 'lye'
  • Vitu vya nywele na urembo

Kemikali zingine zaweza kudhuru mwili wako baada ya matumizi ingawa hautahisi ukiwa mgonjwa. Zingine zitaonyesha madhara hata baada ya matumizi ya kemikali. Madhara mengine huwa ni ya muda mfupi na mengine ni ya kudumu. Kwa mfano:

  • Kuuma na kichwa. kisunzi
  • Kupiga chafya na kukohoa
  • Uozaji wa meno na finzi
  • Maumivu ya kifua na mapafu
  • Shida za maini
  • Shida za fuko la mkojo na figo
  • Shida za ngozi
Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw030113