Je kuharisha ni nini na mbona ni hatari kwa maisha ya mtoto wangu

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Kuharisha kunasababishwa na viini vinavyopatikana haswa kwa kinyesi. Viini hivi huingia kinywani mwa mtoto wakati anapochezea mahali palipo na taka au kinyesi, mahali ambapo usafi haudumishwi, mahali palipo na ukosefu wa maji safi ya kunywa na wakati mtoto mchanga anapokosa kunyonyeshwa vizuri.

Kuharisha husababisha kifo cha mtoto kwa kusababisha upungufu wa maji mwilini. Watoto huwa zaidi katika hatari ya kifo kutokana na kuharisha kuliko watu wazima kwa sababu watoto huishiwa na maji mwilini kwa haraka na tena kuharisha kunaleta utapiamlo. Punde kuharisha kunapoanza mtoto, ni muhimu kumpa mtoto vyakula vya maji maji zaidi pamoja na vyakula vingine vya kawaida.

Mtoto husemekana ana maradhi ya kuharisha wakati kinyesi chake kinaonekana kuwa maji maji mara tatu au zaidi kwa siku. Vile ambavyo kinyesi kinaonekana maji maji zaidi, ndivyo hatari ya maradhi ya kuharisha yalivyo makali.

Baadhi ya watu hufikiria kuwa kunywa maji au vyakula vingine vya maji maji wakati unapo harisha ni vibaya na hufanya kuongezeka kwa makali ya kuharisha. Hiyo si kweli. Mtoto anaye uguwa maradhi ya kuharisha anastahili kupewa maji na vyakula viingine vya maji maji, na hata maziwa ya mama kama bado ni mtoto anayenyonya, mara nyingi kama iwezekanavyo. Hii inasaidia kurejesha mwilini, maji yanayo potea kwa kuharisha.

Sources