kupata usaidizi: Shida za kiakili hummaliza mwanamke nguvu na kumfanya akate tamaa. Kukutana kunaweza kumpa nguvu, ambayo itamsaidia kukabiliana na shida za kila siku.
tambua hisia: wakati mwingine wanawake huficha hisia zao (hawatambui kuwa wanazo) kwa sababu wanafikiri kuwa, hisia ni mbaya, hatari au za aibu. Wanaposikia wengine wakizungumzia hisia zao inaweza kuwasaidia kutambua hisia zao.
dhibiti unavyosuluhisha mambo: Wanachama wanaweza kumsaidia mwanamke kutafakari kuhusu shida ambayo anayo, ili aweze kufanya uamuzi unaofaa.
elewa vyanzo vya mambo: kwa kuzungumza pamoja, wanawake huanza kutambuakuwa, wengi wao wanakabiliwa na changamoto sawa. Hii huwasaidia kutambua chanzo cha shida hizi.
kuwa na suluhu: Suluhu ambazo hujadiliwa kwenye kikundi hukubaliwa na kutumika kwa urahisi kuliko zile ambazo mwanamke atafikiria mwenyewe.
fanyeni mambo kwa pamoja: wanawake wanapofanya mambo kwa pamoja huwa na nguvu zaidi kuliko yule anayefanya mambo peke yake.
Sources
Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.