Je kuna aina zipi za kubakwa na unyanyasaji wa kijinsia

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Kuna aina nyingi za unyanyasaji wa kijinsia. Lakini, ni chache tu ambazo hutambuliwa na watu kama kubakwa. Kwa mfano, wakati mwingine matukio maishani yanaweza kumfanya mwanamke ashiriki ngono hata kama hana nia ya kufanya hivyo. Hii inaweza kutendeka katika ndoa. . Wanawake wengine huishi kwa kuamini kuwa kushiriki ngono ni wajibu wao, watake wasitake. Ingawa serikali haitoi adhabu kwa aina hii ya dhuluma ya kingono, sio halali.

Kwa wanawake wengine, kushiriki ngono ni njia ya kujipatia riziki - ili kuwakimu watoto wao, kupata makao, kupata pesa, au kuwa na ajira. Haijalishi sababu, mwanamke hafai kulazimishwa kushiriki ngono ikiwa hataki.

Katika uhusiano wowote ule, mwanamke anaweza kukubali au kukataa kushiriki ngono. Akikataa, basi mwanamume hana budi ila kuheshimu na kukubali uamuzi wake, na wala asijaribu kumshawishi kubadilisha uamuzi wake, wala kumlazimisha. Hata kama mwanamke huyo anajuana na yule mwanaume na aseme "ndio", hata ingawa hakuwa na uwezo wa kukataa, basi hiyo ni ubakaji.

Mara nyingi, mwanamke huona vigumu kuomba msaada ikiwa anajuana na huyo mwanaume. Ni vigumu zaidi ikiwa itabidi waonane tena.

Wakati wowote mwanamke hulazimishwa kushiriki ngono, kama kuna vurugu au la, inaweza kumsababishia shida nyingi za kiafya na hisia.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020304