Je kuna shida zipi zinazotokana na hedhi

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Ikiwa unashuhudia shida wakati wa hedhi, jaribu kuzungumza na mama yako, dada zako au marafiki. Utagundua kuwa, hata wao wana shida kama zako na wanaweza kukusaidia.

Baadhi ya shida zinazoshuhudiwa mara kwa mara wakati wa hedhi ni:

  • mabadiliko katika hedhi
  • maumivu wakati wa hedhi
  • shida nyinginezo za hedhi

Dalili hatari:

Ikiwa mwanamke anashuhudia mojawapo ya dalili hizi, anahitaji uchunguzi wa kimatibabu haraka iwezekanavyo.

  • kuvuja damu na maumivu upande wa chini wa tumbo, wakati hedhi haijapatikana
  • kuvuja damu wakati wa uja uzito
  • kuvuja damu kupita kiasi baada ya kujifungua, kuharibika kwa mimba au kuavyaa mimba
Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010216