Je mawazo gani kuhusu kula yana madhara
Katika sehemu kadhaa ulimwenguni, tamaduni na itikadi kuhusu wanawake na chakula ni hatari na hazisaidii. KWa mfano:
Si kweli kuwa wasichana wanahitaji chakula kidogo kulika wavulana.
Baadhi ya watu huamini kuwa wavulana wanahitaji chakula zaidi. Watu hawa wamepotoka! Katika jamii nyingi, wanawake hufanya kazi sawa na wanaume, au mara dufu, na wanhitaji kuwa na afya njema. Wasichana wenye afya njema na hulishwa vyema wangali wachanga, huwa wanawake wenye afya njema, na hupata shida kidogo sana shuleni na kazini.
Sio kweli kuwa wanawake wanafaa kuepuka vyakula fualni wakati wao ni waja wazito au wanaponyonyesha.
Katika baadhi ya jamii, watu wanaamini kuwa ni lazima mwanamke ajiepushe na vyakula kama vile maharagwe, mayai, kuku, vyakula vya maziwa, nyama, samakimatunda na maboga -katika nyakati tofauti maishani mwake. Nyakati hizi zinajumuisha wakati wa hedhi, uja uzito, baada ya kujifungua, anaponyonyesha au hedhi inapokomaa. Lakini, mwanamke anahitaji vyakula hivi vyote, hasa akiwa mja mzito na anaponyonyesha. Kuepuka vyakula hivi kunaweza kusababisha uchovu, magonjwa na hata kifo.
Sio kweli kuwa lazima mwanamke ailishe jamii yake kwanza Mara nyingi mwanamke hufundishwa kuilisha jamii yake kwanza kabla ya yeye kula. Mara nyingi yeye hula bakshishi, ambayo mara nyingi hapati chakula sawa na jamii yake. Hii sio lishe bora hata. Hii ni hatari ikiwa mwanamke huyo ni mja mzito au ndio amejifungua.
Ikiwa familia haitamsaidia mwanamke kula vyema, tunahimiza afanye awezalo ili apate lishe bora. Itabidi ale anapotayarisha chakula, au afiche chakula ili aweze kula wakati mumewe hayuko nyumbani.
Sio kweli kuwa mtu anayeugua anahitaji chakula kidogo kuliko aliye mzima Chakula kizuri hakizuii tu magonjwa bali pia humsaidia anayeugua kupigana na magonjwa ili aweze kupona. Vyakula ambavyo ni vizuri kwa watu wakati hawaugui, ni vizuri wakati ambapo wanaugua.