Je mawazo yanawezaje kuharibu afya yangu ya kiakili
Matukio na shughuli za kila siku mara nyingi humshinikiza mwanamke na kufanya mwili wake kuwa na mvutano na wasiwasi akilini. Wasiwasi hii inaweza kutokana na shida za kimwili, kama vile ugonjwaau kazi nyingi. Pia inaweza kutokana na matukio ya kihisia kama vile ugomvi kwenye familia au kulaumiwa kwa shida ambazo zimemshinda mwanamke. Hata matukio yanayoleta raha - kama vile kujaaliwa mtoto au kupata kazi - huleta mvutano kwa sababu huleta mabadiliko katika maisha ya mwanamke.
Wanawake wengi huwa na kila aina ya wasiwasi ambazi huwashinikiza kutoka pande zote:
Ni rahisi kukosa kuona shinikizoambalo huwapata wanawake kila siku ya maisha yao kwa sababu shinikizo huwepo kila siku. Hii huchukua wakati mwingi sana wa mwanamke ili kuweza kukabiliana na shinikizo hizi.
Mwanamke anapokabiliana na shinikizo hizi kila siku na kwa muda mrefu, huenda ataanza kuhisi kam a mambo yamemzidi sana. Shinikizo hili huwa mbaya zaidi ikiwa amefundishwa kuwalinda wengine kwanza na kujishughulikia mwisho. Ule wakati mdogo ambao yeye husalia nao wa kupumzika au kufurahia mambo ambayo yangesaidia kupunguza shinikizo hizi, huenda hatatambua ishara za ugonjwa au kazi nyingi. Kwa kuwa yeye ni mwanamke, hana uwezo wa kubadilisha hali ya mambo yalivyo.
Mara nyingi mwanamke hufanywa kuhisi kuwa yeye ni dhaifu au mgonjwa. Lakini, huenda shida ni kwamba anadhulumiwa maishani. Ili kuwa na afya njema ya kiakili, wanawake wanahitaji udhibiti na uwezo juu ya maisha yao.