Je mtu huuathirika vipi kiakili hapo anapopata hasara au kufiiwa

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Mwanamke anapopoteza kitu au mtu muhimu kwa mfano: ampendaye, kazi, nyumba/boma au Urafiki wa karibu huenda akajawa na huzuni. Hii huweza kutokea pia anapougua au akipata ulemavu fulani.

Huzuni hutokea kawaida na husaidia mtu kuomboleza kifo au hasara aliyoipata. Lakini mwanamke anapopata hasara nyingi kwa pamoja, au akiwa tayari ana matatizo huenda akaanza kuathirika kiakili. Hii pia huweza ikatokea mwanamke anapokosa kuombolezi namna ya kimila. Kawamfano:akiwa amelazimishwa kuhamia mahali mila zake hazitambuliki.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw011504