Je napaswa kumyonyesha mtoto wangu kwa muda gani
From Audiopedia - Accessible Learning for All
Ni vyema kumnyonyesha mtoto wako kwa muda mrefu iwezekanavyo, angalau mwaka mmoja. Katika miezi 6 ya kwanza, usimpe mtoto chochote ila kumnyonyesha tu.
Ikiwa mama anayenyonyesha atashika mimba, anaweza kuendelea kunyonyesha. Ni muhimu mama anayenyonyesha huku akiwa mja mzito kula vyakula vya afya.
Ni salama kuendelea kumyonyesha yule mtoto wa kwanza hata baada ya mama kujifungua. Lakini, yule mtoto mchanga anyonyeshwe kwanza.