Je naweza kuzuia maumivu ya miguu

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Mara nyingi wanawake waja wazito huumwa na miguu - haswa wakati wa usiku, au wanapojinyoosha au kuangalisha vidole vya miguu chini. Ukosefu wa madini aina ya 'calcium' ndio husababisha maumivu ya miguu.

Namna ya kuzuia:

Kula vyakula vingi vya wingi wa madini aina ya 'calcium' kama vile maziwa, jibini, simsim na mboga za kijani.

Ikiwa miguu yako ina maumivu:

  • Angalisha vidole vyako vya miguu juu na kisigino chini.
  • Kisha, sugua miguu yako ili iweze kutulia.
  • Vidole vyako vya miguu VISIASHIRIE chini. Hii hufanya maumivu kuwa makali zaidi.
Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010713